Sunday, 5 April 2015

KANISA KATORIKI KASULU CHINI YA FATHER-DEUS(PAROKO) WALIPOTEMBELEA KITUO CHA WALEMAVU KABANGA.



Paroko,mwenyekiti wa kigango cha Murubona na Kumsenga pamoja na waumini wengine wa Kanisa Katoriki Kasulu mjini,ahsantemi sana kwa kutembelea shule/kituo chetu cha Kabanga na kutoa msaada wenu wa hali na mali na kubwa zaidi mchango wa Tsh.1,700,000/=(Cash.Tsh.1,590,000/= pamoja na ahadi ambazo hutimiza jumla ya kiasi tajwa hapo juu) kwa ajili ya mwanafunzi wetu Gilbert.
Mbarikiwe sana ndugu zetu.
"MOYO USIO NA SHUKRANI HUKAUSHA MEMA YOTE"
 Baadhi ya wanafunzi na wakazi wengine waishio katika kituo cha walemavu Kabanga wakifurahia zawadi walizoletewa na waumini wa Kanisa Katoriki-Kasulu.(4.4.2015)
 Umati wa waumini wa Kanisa Katoriki Jimbo la Kasulu mjini walioambatana na Paroko lakini pia viongozi mbalimbali wa kanisa hilo kuja kuwajulia hali na kuwafariji walemavu wa ngozi(ALBINO) na kuwaletea zawadi kemkem siku moja kabla ya Pasaka (kwa kweli wamevunja rekodi haijawahi kutokea) kutembelewa na umati mkubwa kama huu. TUMEFARIJIKA SANA
Wanaoonekana hapo mbele ni baadhi ya wanakwaya waliotumbuiza na kupamba matembezi haya.Sintosahau wimbo mzuri wa Kiha ulioinua watu ukumbini na kucheza kwa furaha chini ya kwaya masta "Kihekidye"



KARIBUNI TENA KABANGA

No comments:

Post a Comment